Tarehe ya mwisho kusasishwa: Julai 2026
Karibu kwenye Aziry Tech WhatsApp AI Sales Agent (SaaS). Tunachukulia faragha na usalama wa data zako kwa kiwango cha juu zaidi. Mfumo wetu umejengwa kwa misingi imara ya kiusalama kuhakikisha wewe na wateja wako mnakuwa na amani. Kwa kutumia huduma hii, unakubaliana na masharti yafuatayo:
Ujumbe Wako ni Wako Tu. Mfumo huu unatumia mfumo wa usimbaji fiche (encryption) unaohakikisha kwamba hakuna mtu yeyote yule, hata sisi watengenezaji (Aziry Tech), anayeweza kusoma meseji zako na wateja wako. Ujumbe unaingia moja kwa moja kwenye server salama ukiwa umefichwa (encrypted) na kusomwa pekee na wewe (mmiliki halali) na AI inayokuhudumia ukiwa umeruhusu.
Wewe ndiye mmiliki halali asilimia mia moja (100%) wa namba za simu, mawasiliano, na data zote za wateja wako. Mfumo wetu ni daraja tu la kurahisisha mawasiliano. Data zako hazitauzwa, hazitasambazwa, wala kutumiwa na mtu mwingine au kampuni nyingine yoyote nje ya makubaliano haya. Ukiamua kufuta akaunti yako, data zote zitafutwa moja kwa moja kwenye server zetu bila kubakiza nakala yoyote.
Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, Mteja wako anapotuma ujumbe, atapewa uhuru wa kuchagua kuhudumiwa na AI au kuongea na wewe moja kwa moja. Hii inajenga uaminifu na uwazi. Endapo mteja atachagua kuongea na wewe (Rafiki), AI yetu itajizima kiotomatiki kwa mteja huyo.
Unakubali kwamba:
Tunaweza kusasisha masharti haya mara kwa mara ili kuboresha usalama. Tutaweka taarifa hapa yakitokea mabadiliko makubwa.
← Rudi Kujisajili